Dalali ajitosa Uwenyekiti Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Dec 2020
Dalali ajitosa Uwenyekiti Simba

Wakati zoezi la kurejesha fomu za kuwania nafasi ya Mwenyekiti wa klabu ya Simba likitarajiwa kufungwa leo majira ya saa 12 jioni, aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo Hassan Dalali ni miongoni mwa Wanachama walijitosa kwenye kinyan'ganyiro cha kuwania nafasi iliyoachwa wazi na Swedi Mkwabi

Dalali amesema baada ya kuombwa na Wanachana wengi wakimtaka ajitose kugombea nafasi hiyo, ameitikia wito huo na alichukua na kurejesha fomu

Dalali amesema Wanachama wengi wa Simba walifika nyumbani kwake wakimtaka agombee na zaidi waliamua hata kumtolea fedha ya fomu Tsh Milioni Moja

"Nimechukua fomu kutokana na wanachama kunifuata nyumbani kwangu kuhitaji nifanye hivyo ambao wamenichangia fedha ya kwenda kuchukulia fomu kiasi cha shilingi milioni moja (1,000,000).

"Haina shida iwapo mimi nilikuwa mwenyekiti awali kwa kuwa sikuongoza miaka nane mfululizo, kikanuni inaeleza kuwa iwapo umekuwa mwenyekiti kwa muda wa miaka minne kisha ukaishia hapo na ukakaa pembeni na ukihitaji kugombea tena unaruhusiwa.

"Nisingeweza kuruhusiwa kugombea iwapo ningekuwa nimeongoza kwa miaka nane mfululizo, kipindi kile sikuweza kugombea kutokana na vigezo vilivyowekwa vya elimu ya digrii lakini sasa uchaguzi unakwenda kwa mujibu wa kanuni ya TFF ambayo inaruhusu mtu kugombea akiwa na elimu ya kidato cha nne, "amesema Dalali.

Wanachama wengine wa klabu ya Simba wanaotajwa kujitosa kugombea nafasi hiyo ni Mohamed Soloka na Ayubu Semvua

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’