Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema hakufurahishwa na matokeo ya kufungwa bao 1-0 dhidi ya Platinum Fc kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa nchini Zimbabwe
Katika mchezo huo ambao Platinum walifunga bao pekee kwenye dakika ya 17, Sven amesema wachezaji wake walikosa umakini kutumia nafasi walizotengeneza
Aidha kukosa umakini kwa safu yake ya ulinzi, kulipelekea Platinum kufunga bao hilo ambalo limewaweka mbele baada ya dakika 90 za kwanza
"Sijafurahia matokeo sababu hakutustahili kupoteza, tulitawala mchezo na hasa mwanzoni lakini tulikosa umakini kwenye eneo la mwisho ili kufunga. Wamefanikiwa kufunga na hivyo tunapaswa kuwa makini zaidi kwenye mchezo wa marudiano," alisema Sven
Mchezo wa marudiano utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Januri 06 2020 ambapo Simba itahitaji matokeo ya ushindi kuanzia mabao mawili ili iweze kutinga makundi