Simba yapania ushindi Shinyanga

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Feb 2018
Simba yapania ushindi Shinyanga
Vinara wa ligi kuu ya Vodacom, Simba leo wanashuka kwenye uwanja wa Kambarage Shinyanga kuikabili Mwadui FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 18.

Simba inaongoza ligi kwa tofauti ya alama nne dhidi ya wapinzani wao Yanga ambao jana wamepata ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Majimaji hivyo kufikisha alama 37.

Simba itaingia katika mchezo huo ikiwa na lengo la kuibuka na ushindi ili kuhakikisha inarejesha uongozi wake wa alama saba zaidi.

Simba itamkosa mlinzi wake wa kushoto Asante Kwasi anayetumikia adhabu ya kadi tatu za njano. Hii itatoa fursa kwa mchezaji bora wa VPL msimu uliopitwa Mohammed Hussein kurejea kikosini.

Simba iko katika kiwango bora kwani imeshinda michezo saba iliyopita bila ya kuruhusu bao nyavuni kwake.

Kinara wa mabao Emanuel Okwi atakuwa anasaka bao lake la kwanza nje ya jiji la Dar es salaam huku nahodha John Bocco akitarajiwa kuendeleza kasi yake ya kupachika mabao katika viwanja vya mikoani.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
10h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’