Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wanahusishwa kumuwania Mshambuliaji wa Kimataifa wa Nigeria, Junior Sewanu Lokosa mwenye Umri wa Miaka 27
Mshambuliaji huyo alisitishiwa Mkataba kwa makubaliano ya Pande zote na Klabu yake ya mwishso kuitumikia, Esperance de Tunis ya Nchini Tunisia
Akiichezea Kano Pillars, Lokosa alikuwa mfungaji bora katika ligi kuu ya Nigeria "NPFL"msimu wa 2017/18, akifunga mabao 19 katika mechi 21
Lokosa alijiunga na Esperance mnamo 2019, alikuwa na wakati wake mzuri katika nusu ya kwanza ya Mwaka 2019 kabla ya jeraha ambalo lilipunguza Ubora wake katika klabu hiyo ya Tunisia
Alifanikiwa kufunga mabao mawili katika mechi 11 alizocheza kwa Esperance lakini alishinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na ubingwa wa ligi ya Tunisia na klabu hiyo
Mnamo Mei 2018, alienda kufanya majaribio huko Bulgaria Katika Klabu ya Ludogorets, na pia huko Norway Katika Klabu ya Brann
Baada ya kufanya majaribio nchini China, alijiunga na EspΓ©rance Sportive de Tunis mnamo 14 Januari 2019, akitia saini kandarasi ya miaka miwili na nusu. Mnamo Julai 30, 2020 mabingwa hao wa Tunisia walitangaza kuondoka kwa Lokosa kwa kusitisha mkataba wake