Uongozi wa klabu ya Simba umetoa taarifa rasmi kuhusu kuachwa kwa winga Berbard Morrison katika kikosi kilichosafiri nchini Zimbabwe tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc kesho Jumatano
Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema Morrison aliachwa kwa sababu ni mgonjwa
"Morrison alikuwa akisumbuliwa na maradhi, alianza matibabu yake Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hivyo isingekuwa rahisi kusafiri nae"
"Nimezungumza nae, sasa anaendelea vizuri, tunatarajia ataungana na timu pale tutakaporejea jijini Dar es salaam," alisema Barbara
ADVERTISE HERE