Uongozi wa klabu ya Simba umefuta tetesi nyingi zilizokuwa zikiihusisha klabu hiyo na mshambuliaji wa Orlando Pirates Justine Shonga
Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amesema Shonga hayuko katika mipango yao ya usajili
"Justine Shinga sio miongoni mwa wachezaji tunaowataka. Jina lake halimo katika mipango yetu ya usajili"
"Tutaongeza wachezaji katika usajili huu wa dirisha dogo, lakini pia wapo wachezaji tutawatoa kwa mkopo. Taarifa itatolewa baada ya kukamilisha mazungumzo na timu tunazotaka kuwapeleka," alisema Barbara
Shonga raia wa Zambia amehusishwa mara nyingi na klabu ya Simba hata kabla hajatua Pirates
Ni mmoja wa washambuliaji wazuri ingawa kwa sasa hana nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha Pirates
ADVERTISE HERE