Sven kuamua hatma ya Bocco, Manula leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Dec 2020
Sven kuamua hatma ya Bocco, Manula leo

Nahodha John Bocco na mlinda lango Aishi Manula leo watafanyiwa tathmini kama wanaweza kucheza mechi ya ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc ambayo itapigwa kesho Jumatano, uwanja wa Taifa wa Zimbabwe

Akizungumza na wanahabari jana, Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez alisema Bocco na Manula walipata majeraha kwenye mchezo dhidi ya KMC

"Bocco na Manula walipata majeraha kwenye mchezo uliopita dhidi ya KMC. Maendeleo yao yanaridhisha, pengine kocha atatumia program ya mazoezi ya mwisho leo kuangalia utayari wao"

"Wachezaji wengine wote wako kamili, ni Mwalimu mwenyewe ataamua nani amtumie katika mchezo dhidi ya Platinum," alisema Barbara

Aidha Barbara alitoa ufafanuzi kuhusu kiungo Thaddeo Lwanga ambaye walipata changangomoto kupata ITC yake ambapo amesema wanatarajia kuipokea ITC hiyo leo ama kesho wakipambana kuhakikisha wanaipata mapema ili awe sehemu ya kikosi kitakachoikabili Platinum Fc

"Kwa taratibu za nyumbani tulishakamilisha, Lwanga tunaweza kumtumia kwenye ligi. Lakini tulikuwa na changamoto ya kupata kibali chake cha Kimataifa(ITC). Tuliongea na klabu yake ya zamani (Tanta) na mpaka sasa naweza kusema tumekamilisha zoezi hilo kwa asilimia 80"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’