Jumatano hii mabingwa wa nchi Simba SC watakuwa ugenini kuwakabili FC Platinum ya Zimbabwe katika mechi ya mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba wataingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kuingia hatua hii pasipo kuruhusu goli katika mechi mbili za raundi ya awali dhidi ya Plateau United
Mchezo huu utarushwa mbashara na AzamSports1 HD kuanzia saa 10:00 jioni
ADVERTISE HERE