Lwanga kuwakabili Platinum Fc

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Dec 2020
Lwanga kuwakabili Platinum Fc

Kwa mara ya kwanza kocha mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck anatarajiwa kumtumia kiungo mkabaji Thadeo Lwanga kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc ambao utapigwa keshokutwa Jumatano huko Zimbabwe

Mshauri wa Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi, Crescentius Magori amethibitisha kuwa Simba imefanikiwa kupata leseni ya mchezaji huyo ambayo itamuwezesha kushiriki mchezo wa Jumatano kama kocha Sven ataamua kumtumia

Lwanga, kiungo wa Kimataifa kutoka Uganda, alisajiliwa na Simba mwanzoni mwa mwezi huu akiwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba na klabu ya Tanta inayoshiriki ligi kuu ya Misri

Nyota huyo anaweza kuanza sambamba na Jonas Mkude eneo la kiungo

Uwepo wake utampa nafasi Mkude kupanda kuongeza mashambulizi pale Simba inaposhambulia

Lwanga anaonyesha kiwango kizuri katika mazoezi ya Simba wengi wakiwa na matumaini ataitendea haki nafasi aliyopewa

Usajili wake ulikuwa maalum kuchukua nafasi ya Gerson Fraga aliyerejea kwao Brazil kutibiwa jeraha la goti alilopata mwanzoni mwa msimu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
48m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’