Keshokutwa Jumatano katika uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ndipo mchezo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa kati ya Platinum Fc dhidi ya Simba utapigwa
Ni dakika 90 za kwanza kati ya 180 ambazo zitaamua timu ipi inakwenda kucheza makundi
Kwa Simba huu ni mchezo muhimu kuondoka na ushindi au matokeo ya sare ili kujiweka katika mazingira mazuri kuelekea mchezo wa marudiano ambao utapigwa jijini Dar es salaam wiki mbili zijazo
Kikosi cha kocha Sven Vandembroeck jana kiliendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo


ADVERTISE HERE