Kuwasili mapema kwa klabu ya Simba nchini Zimbabwe kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc, kumewaweka katika presha wapinzani wao hao
Mchezo wa kwanza kati ya timu hizo utapigwa Jumatano Disemba 23 na ule wa marudiano kupigwa baada ya wiki mbili jijini Dar es salaam
Simba ilitua Zimbabwe juzi, uongozi wa mabingwa hao wa nchi wakifanya hivyo ili kuwapa wachezaji muda wa kuzoea mazingira na hali ya hewa ya Zimbabwe
Hata hivyo kwa wenyeji wao hali ni tofauti ambapo inaelezwa wanahaha kutuma mashushu kuchunguza mazoezi wanayofanya Simba
Adha nyota Clatous Chama na Luis Miquissone wamekuwa gumzo nchini Zimbabwe, ndio wachezaji wanaozungumzwa zaidi na vyombo vya habari nchini humo
Miquissone yuko katika kiwango bora sana, Wazimbabwe wana kila sababu ya kumuhofia
Simba inafanya mazoezi yake chini ya ulinzi mkali wakihakikisha hakuna mamluki wanaotumwa kufuatilia mazoezi hayo