Simba tayari imetanguliza mguu moja kuekelea hatua ya kwanza kwenye michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika baada ya kuifunga Gendarmerie kutoka Djibouti mabao 4-0.
Hata kama miujiza katika soka ipo, ukweli ni kwamba Wadjibouti hao hawana jeuri ya kugeuza matokeo hayo timu hizo zitakaporudiana February 20 licha ya kwamba watakuwa kwenye dimba lao la nyumbani.
Wakati Simba ikianza kwa ushindi mnono, timu ya Al Masry kutoka Misri nayo imeilaza Green Buffalo ya Zambia mabao 4-0 na hivyo kuwa na uwezekano mkubwa kwa Simba kukutana na Mafarao hao kutoka Misri.
Tayari benchi la ufundi la Simba limeanza kufuatia rekodi ya Al Masry inayonolewa na mkongwe Hossam Hassan.
Kocha Msaidizi wa Simba Masudi Djuma amesema tayari wamepata mikanda ya video ya Al Masry na licha ya kukiri kuwa waarabu hao ni wazuri, lakini amebaini wanafungika.
“Tumewaona kupitia mikanda ya video, si timu ndogo. Tunajua wameshinda mabao 4-0 kama sisi, lakini tuna wachezaji mahiri ambao wana kiu ya kuweza kukabiliana na timu yoyote na tunaomba Mungu atusaidie,†alisema Djuma.
“Tunajua kadiri tunavyozidi kusonga mbele ndivyo tunavyokabiliana na timu ngumu, El Masry ina kikosi kizuri na inatoka kwenye nchi inayotamba katika soka Afrika, lakini hata sisi si wa kubezwa, tuna kikosi imara na kipana, tutapambana na Inshallah tutashinda,†alisema.

ADVERTISE HERE