Wiki ijayo, Rais wa Shirikisho la soka duniani (FIFA), Giovanni Vincenzo atakuwa nchini Tanzania ambapo pamoja na mambo mengine atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli.
Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dk. Harrisons Mwakyembe ametoa taarifa hiyo jana katika Mkutano na Wahariri wa vyombo vya Habari Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
Mwakyembe amesema Serikali imejipanga kuupa mapokezi mazuri msafara wa Infantino ambaye ataongozana na Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Ahmad.
Waziri Mwakyembe amesema kwamba Serikali imeona ugeni huo ni mzito na haiwezi kuliachia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) peke yake kuratibu ziara hiyo.
“Kwa sababu hiyo tumeona tufanye kazi bega kwa bega na TFF ili kuhakikisha Infantino na msafara wake wanafurahi ziara hiyo,â€amesema Mwakyembe
Infantino anatarajiwa kuwasili nchini Februari 20 pamoja na makamu wake Mkuu, David Chung na viongozi wengine wakiwemo wa mabara, Salman Bin Ibrahim Al-Khalifa, Aleksander Ceferin, David Gill, Alejandro Dominguez, Victor Montagliani na Katibu Mkuu, Fatma Samoura.
Kwa mujibu wa Rais wa TFF, Wallace Karia, ujumbe huo unakuja kwa ajili ya Semina maalum ya FIFA itakayohusisha nchi 21, wakiwemo wenyeji, Tanzania, ambayo itadumu hadi Februari 23.
Mapema Rais wa TFF, Karia alizungumzia namna walivyojipanga vizuri kwa ziara hiyo na akasema hayo ni matunda ya uongozi wake mzuri ulioivutia FIFA hadi kuja kuuleta mkutano huo Tanzania.
Kwa upande wake, Mwenyekiti mpya wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodegar Chilla Tenga ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati mbalimbali za CAF amesema kwamba ugeni unaokuja nchini ni wa wasimamizi wakuu wa mchezo wa mpira wa miguu.
“Tuwaonyeshe tumefurahia ujio wao, wamekuja kwetu kwa sababu ya imani, wameona Watanzania wanapenda mpira wanathamini mchango wa FIFA na CAF na wanakwenda sawa na imani yao,â€.
“Wangependa kuona soka ya vijana na kinamama zinaendelea, wangependa kuona kuna nidhamu katika uongozi, haswa nidhamu ya matumizi ya fedha. Hayo yanafanana na sera za nchi yetu kwa sasa,â€amesema Tenga.

ADVERTISE HERE