Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck ana kazi ya kufanya kuhakikisha Simba inafikia malengo yake katika michuano ya ligi ya mabingwa
Baada ya kuvuka hatua ya awali, raundi inayofuata itakuwa ngumu zaidi kwani kila timu inafahamu, ushindi katika raundi hiyo utawapeleka hatua ya makundi
Kumekuwa na hofu miongoni mwa mashabiki wa Simba kutokana na mwenendo wa kikosi chao hasa katika mechi za karibuni pamoja na kuwa ushindi unapatikana
Ile kasi ambayo Simba imekuwa nayo, inapungua mchezo hadi mchezo, morali ya wachezaji imeshuka sana
Kumekuwa na ukosoaji kwenye mbinu anazotumia, hasa uamuzi wa kutumia mshambuliaji mmoja
Wanasimba wanafahamu ubora wa timu yao, Simba hii sio sawa na ile iliyotinga makundi na kucheza robo fainali misimu miwili iliyopita
Malengo yaliyowekwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu ni angalau kufika hatua ya nusu fainali
Jambo hilo litakuwa gumu kutekelezeka iwapo Sven ataendelea na mbinu hizi hizi anazotumia kwenye ligi
Disemba 22 Simba itakuwa ugenini kule Zimbabwe kumenyana na Platinum Fc katika mchezo wa kwanza, raundi ya kwanza na marudiano kupigwa jijini Dar es salaam wiki mbili baadae
Platinum Fc sio timu ya kutisha lakini ni lazima Simba iwe kwenye ubora wake ili kuhakikisha inashinda mchezo huo na kutinga makundi