Saa moja jioni mabingwa wa Taifa hili Simba watashuka pale uwanja wa Benjamin Mkapa kupepetana na KMC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Simba itakuwa ikisaka alama tatu muhimu katika kampeni yao ya kuwania ubingwa wa nne mfululizo
Lakini mashabiki watakaoingia uwanjani mapema, wataanza kwa kushuhudia mchezo mkali wa utangulizi kati ya akina dada wa Simba Queens dhidi ya wenzao Allince Girls
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa kumi jioni hivyo Wanamsimbazi wameaswa kuchangamkia kununua tiketi mapema kupitia vituo vilivyotangazwa mapema

ADVERTISE HERE