Dirisha dogo la usajili kwa msimu wa 2020/21 limefunguliwa saa sita usiku wa kuamkia leo Disemba 16
Dirisha hilo litafungwa Januari 15 2021, saa 5:59 usiku
Ni wakati mwingine kwa timu za ligi kuu, daraja la kwanza na la pili kuimarisha vikosi vyao katika mapambano ya kuwania mataji msimu huu
Mabingwa watetezi ligi kuu ya Vodacom Simba wamesajili mchezaji mmoja tayari, Mganda Thadeo Lwanga ambaye anaweza kuanza kutumika leo mchezo dhidi ya KMC
Maboresho mengine yanatarajiwa kutegemeana na mapendekezo ya kocha Sven Vandenbroeck
ADVERTISE HERE