Mabingwa watetezi ligi kuu ya Vodacom Simba leo watakuwa pale uwanja wa Benjamin Mkapa kuwapa burudani mashabiki wao katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC
Mchezo huo utaunguruma kuanzia saa moja usiku
Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo uliopita, vijana wa Sven Vandenbroeck wataingia katika mchezo huo wakiwa na malengo ya kuendeleza wimbi la ushindi ili kuendelea kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya watani zao Yanga wanaoongoza ligi wakiwa na alama 37
Simba wanaingia katika mchezo huo wakiwa kamili, nyota kama Luis Miquissone ambaye alipumzishwa mchezo uliopita, atakuwa tayari kurejea
Lakini pia mshambuliaji Chris Mugalu aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu, mchezo uliopita alirejea, bila shaka leo atakuwa na dakika zake
Nahodha John Bocco, Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka', Jonas Mkude, Bernard Morrison na nyota wengine wote wako fiti kuelekea mchezo huo
Pengine Wanamsimbazi leo wanaweza kumshuhudia kiungo mpya Thadeo Lwanga akianza kuwatumikia mabingwa hao wa nchi baada usajili wake kukamilishwa
Viingilio vya mchezo huo VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B ni tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Β