Manula aahidi shoo ya kibabe dhidi ya KMC kwa Mkapa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Dec 2020
Manula aahidi shoo ya kibabe dhidi ya KMC kwa Mkapa

Mlinda lango namba moja wa Taifa hili pamoja na klabu ya Simba Aishi Manula amewaalika mashabiki uwanja wa Benjamin Mkapa kesho Jumatano kushuhudia buradani ya kibingwa kutoka kwa timu yao katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya KMC

Manula amesema wakiwa na malengo ya kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo, matokeo ya ushindi ndio ahadi wanayoitoa kwa mashabiki ili kuhakikisha wanapunguza tofauti ya pointi dhidi ya watani zao Yanga

Aidha Manula amesema mchezo huo ni sehemu ya maandalizi ya kikosi kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc ambao utapigwa wiki ijayo kule nchini Zimbabwe

"Tunajua utakuwa mchezo mgumu na wenye ushindani kwa sababu tunaamini KMC ni timu nzuri. Lakini kulingana na malengo yetu ni kutetea ubingwa kwa msimu wa nne mfululizo hivyo tunachohitaji siku ya kesho ni matokeo ya ushindi tu," alisema Manula

"Mashabiki waje kwa wingi washuhudie burudani, huu ni mchezo ambao sisi tuko nyumbani, tunacheza katika uwanja wa Mkapa sehemu ambayo tumeizoea hivyo tumewaandalia mashabiki wetu burudani nzuri"

"Pia ni mchezo ambao utatupa taswira kuelekea mchezo wetu wa ligi ya mabingwa, hivyo tutacheza katika ubora ambao mashabiki wetu wamezoea kutuona"

Simba iko kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 29, alama nane nyuma ya Yanga inayoongoza ligi

Hata hivyo Simba ina mechi mbili za viporo, mchezo dhidi ya KMC ukiwa moja ya mechi hizo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
6h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
6h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
9h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
14h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’