Simba imeomba mapitio ya hukumu ya Kichuya

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Dec 2020
Simba imeomba mapitio ya hukumu ya Kichuya

Klabu ya Namungo FC imetoa ufafanuzi baada ya wadau wengi kuonekana wakihoji kuhusu klabu hiyo kumtumia mchezaji Shiza Kichuya ambaye siku za karibuni zilitoka taarifa kutoka FIFA kwamba klabu ya Simba imepigwa faini kwa kumtumia mchezaji huyo kinyume na taratibu za usajili

Zilikuwepo pia taarifa kwamba, Kichuya amefungiwa kucheza kwa miezi sita kutokana na sakata lake la usajili kutoka Pharco kwenda Simba

Afisa habari wa Namungo FC Kindamba Namlia amesema Kichuya ataendelea kuitumia Namungo Fc wakati shauri hilo likisikilizwa upya na FIFA baada ya Simba kuomba mapitio ya hukumu ya awali

Aidha Kindamba amefafanua kuwa adhabu ya Kichuya ingeweza kuanza baada ya siku 45 kama Simba isingelipa faini kama ilivyoagizwa na FIFA

"Kichuya ataendelea kutumiwa na klabu yake kwa sababu klabu ya Simba imeomba FIFA kufanya mapitio upya ya shauri linalomhusu Kichuya"

"Katika taarifa tuliyopewa kuhusu Kichuya inasema, Kichuya anaweza kufungiwa miezi sita endapo klabu ya Simba itashindwa kulipa faini ndani ya siku 45"

"Mshtakiwa namba moja kwenye shauri lile Shiza Kichuya anaweza kufungiwa miezi 6, mshtakiwa namba mbili Simba SC inaweza kufungiwa kusajili kwa misimu mitatu (madirisha matatu makubwa ya usajili).

"Kwa sasa Simba imeomba mapitio ya hukumu iliyotolewa na FIFA, kwa maana hiyo kila kitu kinaanza upya hadi mapitio yatakapokamilika. Maana yake hata ule muda iliopewa Simba kulipa faini hauangaliwi hadi pale mapitio yatakapokamilika"

"Taarifa itakayotoka baada ya mapitio ndio itafanya kazi. Sisi tunajitahidi kwenda kiwekedi, baada ya kuipata taarifa kuhusu Kichuya mtu wetu wa sheria hakuwepo kwa hiyo tulisubiri hadi asome nyaraka za taarifa tuliyopewa kuhusu Kichuya na atupe tafsiri yake," alisema Kindamba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’