Jana kamati ya saa 72 ilitoa maamuzi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutolea maamuzi kuhusu tukio la Mau Bofu kumpiga Okwi.
Mau Bofu amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Tsh. 500,000 (laki tano) kwa kumpiga kiwiko Emmanuel Okwi katika mechi hiyo iliyofanyika Februari 4, 2018 kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Adhabu hiyo imezingatia Kanuni ya 37(3) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Wachezaji.
Katika mchezo huo ambao Simba iloishinda kwa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Bofu alimpiga kiwiko Okwi tukio lililopelekea apoteze fahamu kwa dakika kadhaa uwanjani.

ADVERTISE HERE