Mabingwa watetezi ligi kuu ya Vodacom Simba wamebakia nafasi ya pili huku wakiwa na mechi mbili mkononi baada ya Azam Fc kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Namungo Fc
Azam imefikisha alama 28 baada ya kushuka dimbani mara 15 wakati Simba yenye alama 29 bado ina mechi mbili za viporo, inashika nafasi ya pili
Hesabu za kocha Sven Vandenbroeck sasa ni kuhakikisha anasogea pale juu ambapo 'Gongowazi' wamepakalia kwa muda...!

ADVERTISE HERE