Mchakato wa uchaguzi Simba waanza leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Dec 2020
Mchakato wa uchaguzi Simba waanza leo

Jana klabu ya Simba ilitangaza kuanza kwa mchakato wa uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wake, Swedi Mkwabi.

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya Simba, Boniface Lihamwike aliwaambia waandishi wa habari Dar es Salaam kuwa uchaguzi huo umepangwa kufanyika Februari 7, 2021

Mkwabi alijiuzulu nafasi hiyo mwaka juzi kwa madai ya kutingwa na shughuli zake binafsi na nafasi yake kukaimiwa na mwanachama wa siku nyingi wa Simba, Mwina Kaduguda

"Uchaguzi utakuwa mdogo wa kuziba nafasi moja ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Simba Mkwabi kwa hiyo inahitajika kuziba nafasi yake kwa kuzingatia kanuni na taratibu kuhakikisha anapatika kiongozi aliyechaguliwa na wanachama"

"Uchaguzi utafanyika Februari 7/2021, nawaahidi wapenzi na mashabiki wa Simba utakuwa huru na wa haki, tutasimamia kanuni zote kwa kuzingatia Katiba ya Simba na za Shirikisho la Soka (TFF)," alisema Lihamwike

Naye Makamu Mwenyekiti wa amati hiyo, Steven Ali alisema mchakato huo ulianza jana kwa wanachama wanaohitaji kuwania nafasi fomu zinaanza kutolewa kuanzia leo hadi Desemba 23

"Kwa siku hizo Desemba 14-hadi 23 fomu zitatolewa na kurudishwa na kuanzia Desemba 27 hadi 28 kamati itakuwa kwenye majukumu ya ndani kufanya usahili kwa wanaowania," alisema Ali.

Pia alisema Desemba 29 hadi 30 kamati hiyo itaweka hadharani majina yaliyopitishwa na Januari 2/2021 ni siku ya kupokea na kupitia mapingamizi yaliyokidhi vigezo kwa wagombea.

"Januari 3/2021 ni siku ya kutoa maamuzi na siku itakayofuata kutangaza majina ya wagombea watakaopitishwa na kamati wakati Februari 5 hadi 6 /2021 kipindi cha kampeni na siku itakayofuatia ni uchaguzi" alisema

Ali alisema gharama za kuchukua fomu ni Sh 30,000 na vigezo vya mgombea kama inavyoeleza kwenye Katiba ya Simba kwenye ibara ya 27 lazima awe mwanachama hai na elimu ya stashahada inayotambulika na Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU)

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
18h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
21h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’