Bao la nahodha John Bocco alilofunga kwenye dakika ya 32 lilitosha kuihakikishia Simba ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliopigwa uwanja wa Sokoine
Hilo lilikuwa bao la nane kwa Bocco msimu huu akiongoza orodha ya vinara wa mabao
Haukuwa mchezo mwepesi kwani vijana wa Mbeya City walitoa upinzani mkali kwa mabingwa hao wa nchi
Aidha Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck alichanga karata zake vyema kwani aliwapa mapumziko baadhi ya wachezaji ili kuhakikisha kikosi chake kinakuwa sawa kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Platinum Fc ambao utapigwa wiki ijayo
Ushindi huo umeipandisha Simba kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 29



ADVERTISE HERE