Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba jioni ya leo kitashuka uwanja wa Sokoine mkoani Mbeya kuikabili Mbeya City katika mchezo wa ligi kuu
Huu ni mchezo muhimu kwa Simba kuhakikisha inaondoka na alama zote tatu ili kupunguza tofauti ya pointi dhidi ya watani zao Yanga ambao ushindi dhidi ya Mwadui Fc umewafanya wafikishe alama 37
Simba ilikamilisha maandalizi yake ya mwisho jana uwanja wa Sokoine kocha Sven Vandenbroeck akiwahakikishia Wanamsimbazi kuwa wamejipanga kushinda
Mashabiki wa Simba leo huenda wakamshuhudia dimbani mshambuliaji Chris Mugalu ambaye alikuwa nje kwa wiki kadhaa kutokana na majeraha
Sven amesema Mugalu amepona na anaweza kumpa nafasi kwenye mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 1o Alasiri
Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imekusanya alama 26, ushindi leo utawafanya wapande juu kwenye nafasi ya pili