Hatutawadharau Mbeya City - Sven

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Dec 2020
Hatutawadharau Mbeya City - Sven

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema watahitaji kuwa kwenye ubora wao hapo kesho Jumapili katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbeya City ili waweze kuondoka na alama zote tatu

Sven aliyesafiri mkoani Mbeya na kikosi cha wachezaji 21, amesema hawapaswi kuwadharau Mbeya City kwani wamekuwa na mwenendo mzuri katika michezo mitano iliyopita

Mbelgiji huyo amesema wachezaji wake wote wako katika hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao utapigwa uwanja wa Sokoine

"Tumekuja na wachezaji 21 na wote wapo tayari kwa mchezo. Mbeya City ni timu hatari, hawajapoteza kwenye michezo mitano iliyopita hivyo kesho lazima tuwe vizuri zaidi ili tuweze kuibuka na ushindi," amesema

Simba imekamilisha maandalizi yake ya mwisho dimba la Sokoine tayari kwa mchezo huo ambao matokeo ya ushindi ni muhimu zaidi kwa mabingwa watetezi

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
2h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
16h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
20h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
2d ago
READ MORE β†’