Habari ya uhakika kutoka chanzo makini ndani ya uongozi wa Simba ni kuwa matajiri kutoka nchini Misri klabu ya Pyramids Fc, wameweka mezani ofa kwa ajili ya kumsajili kiungo mshambuliaji Luis Miquissone
Pyramids wako tayari kumn'goa Miquissone kwa kitita kinachokadiriwa kufikia Tsh Bilioni 1.7
Fedha hizo ni zaidi ya mara ya mbili ya kitita ambacho Simba walitumia kumsajili Miquissone kutoka Mamelodi Sundowns (Tsh Milioni 700)
Kutokana na kiwango cha juu anachoonyesha Miquissone sasa, ni wazi timu nyingi zitapigana vikumbo viunga vya Msimbazi kuiwania saini yake
Habari njema ni kuwa bado ana mkataba wa miaka miwili na nusu na Simba, hivyo mabingwa hao wa nchi wakiamua kumuuza watanufaika zaidi
Β
ADVERTISE HERE