Sven ataja sababu ya mabadiliko ya kikosi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Dec 2020
Sven ataja sababu ya mabadiliko ya kikosi

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amesema suala la mabadiliko ya kikosi kutoka mechi moja na nyingine haliepukiki kutokana na changamoto ya ratiba

Juzi Mbelgiji huyo alitupiwa lawama kufuatia uamuzi wake wa kuwaacha nje baadhi ya wachezaji kwenye mchezo dhidi ya Polisi Tanzania ambapo mabadiliko aliyofanya kwenye kipindi cha pili ndiyo yaliyoihakikishia Simba ushindi kupitia kwa Clatous Chama

Hata Sven amesema ratiba inawalazimu kufanya 'rotation' ya wachezaji kwani kuna wakati wanacheza kila baada ya siku tatu

"Kikosi changu ni kipana, nina uwezo wa kuwapanga wachezaji 11 watakaoanza lakini kwenye benchi nitakuwa na wengine saba ambao wana uwezo kama waliokuwa ndani na wakanipa machaguo mengine tofauti ya kucheza"

"Kwa mechi ya juzi sitaacha kumpongeza Clatous Chama. Ukiachana na upana wa kikosi, mabadiliko mengine yanatokeaa kwa sababu ndani ya mwezi huu kila baada ya siku tatu tutakuwa tunacheza mechi kwa maana ilikuwa lazima wengine wapumzike na kutumia wengine," alisema

Baada ya mchezo wa Jumatano, Simba itashuka tena uwanjani Jumapili, kuikabili Mbeya City kule mkoani Mbeya kisha watarejea jijini Dar es salaam tayari kwa safari ya Zimbabwe kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa raundi ya kwanza dhidi ya Platinum Fc

Mchezo huo utapigwa Disemba 22-23 na marudiano kupigwa wiki mbili baadae jijini Dar es salaam

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
8h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’