Sven ampa tano Mzamiru

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
10 Dec 2020
Sven ampa tano Mzamiru

Kocha Mkuu wa Simba Sven vandenbroeck ameeleza kuridhishwa na kazi kubwa inayofanywa na kiungo Mzamiru Yassin katika michezo aliyompa nafasi ukiwemo wa jana dhidi ya Polisi Tanzania ambao Simba ilishinda mabao 2-0

Sven amesema Mzamiru ndiye mchezaji anayekimbia zaidi uwanja kuliko wachezaji wengine, hufanya kazi zaidi ya wachezaji wote anapokuwa uwanjani

"Nampongeza sana Mzamiru, ukiangalia namna anakimbia uwanjani ni zaidi ya wote na anafanya kazi nzuri sana katika kukaba. Anaweza kukosa pasi kadhaa lakini muda mwingine lazima utegemee hilo sababu anafanya kazi nyingine kwenye timu ambayo ni muhimu zaidi," amesema Sven

Tangu alipotua msimu wa 2016/17, Mzamiru amejijengea heshima na jina kutokana na aina yake ya uchezaji

Baadhi ya wachambuzi waifikia hatua ya kumpachika jina la kiungo 'Punda'

Ni kwa sababu hucheza bila ya kuchoka na hujitoa sana katika kuisaidia timu

Ni bahati mbaya hutokea nyakati baadhi ya mashabiki huwa hawaioni kazi yake uwanjani lakini yeye ni mchezaji aliyejipambanua na makocha wengi waliopita Simba wamemtumia katika vikosi vyao

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
31m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’