Nahodha wa Simba John Bocco ameshangazwa na kuenezwa kwa uzushi uliotokana na video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii jana baada ya mchezo dhidi ya Polisi Tanzania, mchezo ambao Simba ilishinda kwa mabao 2-0
Kipande cha video hiyo, kilionyesha kama Bocco alikuwa akimkwepa Kagere wakati wachezaji wa Simba wakipongezana baada ya Chama kufunga bao
Hata hivyo sehemu ya video hiyo ni kama ilikatwa na kuonyesha wakati Bocco anaondoka eneo la tukio hivyo wengine kutafsiri kuwa alikuwa akimkwepa Kagere
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Bocco ameeleza kushangazwa na uvumi huo kwani hakuna tofauti yoyote kati yake na Kagere
Aidha amewashukia baadhi ya wachambuzi wa soka nchini ambao wanajaribu kutengeneza matukio ili kuvurugu amani na utulivu uliopo ndani ya klabu ya Simba
"Hatuna tofauti yoyote na Meddie tupo sawasawa. Walicho kitafsiri watu ni mihemko yao ya kilasiku yakukosa habari na kutaka kutengeneza story zisizo na kichwa wala migu"
"Sina shida na Meddie na wala Meddie hana shida na mimi pia. Kagere na timu yetu hatuna tatizo lolote ni amani na upendo hizo zilikua fikra na hisia za watu kutafsiri na kuhisi vitu visivo kuwa na uhalisia na uwakika," aliandika Bocco