Kiungo mshambuliaji wa Simba Francis Kahata amesema hakuna ukweli wowote kuhusu tetesi zinazomuhusisha kurejea klabu ya Gor Mahia kwa mkopo
Kahata amekuwa na wakati mgumu kupata nafasi kwenye kikosi cha kocha Sven Sven vandenbroeck
Hata hivyo amesisitiza kuwa yuko tayari kupigania namba kwenye kikosi cha Simba, lengo lake likiwa kumaliza mkataba
"Nimeziona taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Simba wanakusudia kunitoa kwa mkopo, taarifa hizi sio sahihi. Mimi ni mchezaji halali wa Simba, bado nina mkataba na nitaendelea kujituma kuhakikisha namaliza mkataba Simba"
Kahata alijiunga na Simba Julai 2019 akitokea klabu ya Gor Mahia. Alikuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha Simba wakati wa kocha Patrick Aussems lakini chini ya Sven, hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza