Lwanga ajipanga kupigania namba Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
9 Dec 2020
Lwanga ajipanga kupigania namba Simba

Kiungo mpya wa Simba sc Mganda Taddeo Lwanga amesema kuwa klabu hiyo ina viungo wengi wazuri lakini anaamini kuwa atapambana na kufanikiwa kupata nafasi katika kikosi Cha klabu hiyo

Lwanga aliyesajiliwa na Simba wiki iliyopita kuchukua nafasi ya majeruhi Gerson Fraga, amesema anafahamu atahitaji kupambana ili kuweza kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza

"Nimeona Simba kuna viungo wengi wazuri na mpaka unapata nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza au kuingia kuna kazi kubwa ambayo mchezaji unatakiwa kuifanya katika mazoezi ili kupewa mechi," alisema mchezaji huyo wa zamani wa Tanta ya Misri.

"Ukiangalia katika mechi na Plateau nafasi ya kiungo mkabaji walicheza Jonas Mkude na Mzamiru Yassin ambao walitimiza majukumu vizuri ya kazi yao, lakini ukiachana na hao kuna viungo wengine kama Said Ndemla na Larry Bwalya hawakutumika lakini wapo katika viwango bora.

"Ubora wa viungo na wachezaji wote wa Simba nalifahamu hilo na nipo tayari kwa kushindana na kuna kitu ambacho nitajitahidi kuongeza katikati kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara, kwani wote tuna malengo ya kuhakikisha tunapambana kwa ajili ya timu na kuifikisha mbali,"  aliongeza Lwanga

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
9h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
9h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
12h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’