Shirikisho la soka duniani (FIFA) limemfungia aliyekuwa mchezaji wa Simba na Pharco ya Misri Shiza Kichuya kwa Kosa la kuihama klabu yake ya Pharco bila kupata ruhusa kutoka kwa kiongozi yeyote.
Klabu yPharco imemshtaki Kichuya FIFA baada ya kuondoka bila kufuata taratibu za uhamisho.
Kichuya tayari ameshachezea klabu mbili za Tanzania bila ya kuwa na kibali cha uhamisho (release Letter) ambazo ni Simba na sasa Namungo Fc
Aidha, klabu ya Simba imeepuka adhabu ya kufungiwa usajili lakini imekumbana na faini ya dola za Kimarekani 130,000 ambazo ni sawa na zaidi ya Shillingi Milioni 300 Za Kitanzania.
ADVERTISE HERE