Mo ateta jambo na Miquissone

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Dec 2020
Mo ateta jambo na Miquissone

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' leo alifanya mazungumzo na winga hatari wa mabingwa hao wa nchi Luis Miquissone

Miquissone kwa sasa ndio habari ya mjini kutokana na kiwango cha juu alichokionyesha katika michezo ya hivi karibuni

Mo amesema baada ya mazungumzo yao, Wanamsimbazi watarajie mambo mazuri zaidi kutoka kwake

"Nimepata wasaa wa kuzungumza na Luis Muiquissone aliponitembelea leo ofisini. Tutegemee mpira wenye ufundi na chenga nyingi zenye kutuletea shangwe," aliandika Mo kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

Miquissone alitua Simba usajili wa dirisha dogo msimu uliopita akiwa bado na mkataba wa miaka miwili na nusu

Inaelezwa Simba imeanza mazungumzo nae ili kumpa mkataba wa muda mrefu zaidi kwani kutokana na umahiri wake ni wazi timu nyingi zitapiga hodi Msimbazi kuitaka saini yake

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
5h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
11h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
14h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’