Mo ampa mtihani Sven

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Dec 2020
Mo ampa mtihani Sven

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba na mwekezaji wa timu hiyo, Mohamed Dewji ‘Mo’, amesema licha ya timu yake kufanikiwa kutinga hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hajafurahishwa na ubutu wa safu ya ushambuliaji na kusema kocha Sven Vandenbroeck anahitaji kufanyia kazi

Mo alisema jambo kubwa lilikuwa ni kupata nafasi ya kufuzu hatua inayofuata na hilo lilifanikiwa, ingawa bado kuna tatizo kwa washambuliaji kushindwa kufunga mabao ya kutosha na kuongeza kuwa bao moja walilopata ugenini ndilo ambalo liliwabeba.

Simba walitoka suluhu na Plateau United, Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na kufanikiwa kusonga mbele kwenye hatua inayofuata kwa faida ya bao la ugenini walilopata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa nchini Nigeria wiki iliyopita.

"Kiukweli nashukuru kwanza kwa kuwa tumefanikiwa kufuzu hatua inayofuata, ila ukweli ni kwamba sijafurahishwa na eneo la ushambuliaji kwa kushindwa kufunga mabao ya kutosha, nafi kiri mwalimu na benchi la ufundi wanatakiwa kulifanyia kazi hilo.

"Kama tusingepata bao kule ugenini, basi huenda hali ingekuwa mbaya kwetu. Kuna haja ya kufanyia kazi upungufu huo mapema kwani tunakokwenda ni pagumu zaidi," alisema Mo.

Safu ya ushambuliaji ya Simba iliyocheza dhidi ya Plateau ni John Bocco na Meddie Kagere ambaye juzi alicheza dakika mbili tu baada ya kuingia dakika ya 90 na mashabiki kulalamika kwa nini aliachwa nje ya uwanja kwa muda mrefu kiasi hicho

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
30m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’