Kiungo mpya wa Simba Thadeo Lwanga jana alianza rasmi majukumu yake na mabingwa hao wa nchi kwa mara ya kwanza akishirikia mazoezi yaliyofanyika uwanja wa Mo Simba Arena
Kiungo huyo mkabaji wa Kimataifa kutoka Uganda, ametua Msimbazi kuchukua nafasi ya Gerson Fraga ambaye majeraha aliyopata yatamuweka nje kwa zaidi ya miezi sita
Fraga alifanyiwa upasuaji wa goti mwanzoni mwa wiki iliyopita nchini Brazil
Lwanga amesajiliwa na Simba kwa ajili ya michuano ya Kimataifa lakini wiki ijayo dirisha dogo la usajli litakapofunguliwa, atajumuishwa kwenye kikosi kinachoshiriki ligi kuu

ADVERTISE HERE