Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck amewataka wachezaji wake kucheza kwa tahadhari kuhakikisha wanashinda mechi kuweza kurejea nafasi za juu katika msimamo wa ligi
Mbelgiji huyo amesema baada ya kufanikiwa kuvuka hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa, wanapaswa kuhamishia nguvu zao ligi kuu wakiwa na mechi tatu za viporo
Mchezo wa mwisho wa ligi kuu Simba ilishinda mabao 7-0 dhidi ya Coastal Union, keshokutwa Jumatano mabingwa hao watetezi watashuka uwanja wa Mkapa kuikabili Polisi Tanzania
"Baada ya mechi dhidi ya Plateau United, katikati ya wiki tutakuwa na mechi ya ligi, sasa hapo kwa namna yoyote ni lazima wachezaji wacheze kwa tahadhari"
"Lengo kwenye mechi zetu za ligi ni kuendeleza kasi ile ambayo tuliishia kwenye mchezo wa mwisho ili kupunguza pointi ambazo tumezidiwa na wapinzani wetu
"Tunatambua kwamba tuna kazi ya kutetea ubingwa, hilo halitawezekana ikiwa tutashindwa kupata matokeo mazuri," alisema Sven
Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 23 baada ya kushuka dimbani mara 11
Vinara wa ligi hiyo ni Yanga wenye alama 34 baada ya kushuka dimbani mara 14