Plateau United bado wanamuota Miquissone

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Dec 2020
Plateau United bado wanamuota Miquissone

Beki mahiri wa Plateau United, Denis Nya amemsifu kiungo mshambuliaji  Simba Luis Miquissone kuwa aliwapa wakati mgumu katika mechi zote walizocheza na Simba katika hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Miquissone ndiye aliyetengeneza bao pekee lililofungwa na Simba kule Nigeria likiwekwa kimiani na Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka'

Katika mchezo wa marudiano uliopigwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam, Miquissone alikuwa mwiba mkali kwa walinzi hao wa Plateau

Beki huyo amemtaja Miquissone kuwa angeweza kuwasababishia madhara zaidi kama wasingekuwa makini

"Ilikuwa mechi ya ushindani kwa kila timu, tulikuja kutafuta matokeo, ila bahati haikuwa kwetu, lakini mchezo ulikuwa mzuri tunawapongeza Simba kwa kusonga mbele katika michuano hii"

"Wachezaji wote walifanya majukumu yao ila aliyevaa jezi namba 11 (Miquissone), alikuwa hatari sana kwetu kwa sababu ametengeneza nafasi nyingi"

"Kwenye soka kuna matokeo matatu, tunakubali na sasa tunarejea nyumbani," alisema Nya

Miquissone alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo ambao uliwashuhudia Simba wakitinga raundi ya kwanza na sasa wakiwasubiri Platinum Fc tayari kwa mchezo wa kwanza ambao utapigwa nchini Zimbabwe Dusemba 23

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
11h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
15h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
21h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’