Beki mahiri wa Plateau United, Denis Nya amemsifu kiungo mshambuliaji Simba Luis Miquissone kuwa aliwapa wakati mgumu katika mechi zote walizocheza na Simba katika hatua ya awali michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Miquissone ndiye aliyetengeneza bao pekee lililofungwa na Simba kule Nigeria likiwekwa kimiani na Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka'
Katika mchezo wa marudiano uliopigwa mwishoni mwa wiki jijini Dar es salaam, Miquissone alikuwa mwiba mkali kwa walinzi hao wa Plateau
Beki huyo amemtaja Miquissone kuwa angeweza kuwasababishia madhara zaidi kama wasingekuwa makini
"Ilikuwa mechi ya ushindani kwa kila timu, tulikuja kutafuta matokeo, ila bahati haikuwa kwetu, lakini mchezo ulikuwa mzuri tunawapongeza Simba kwa kusonga mbele katika michuano hii"
"Wachezaji wote walifanya majukumu yao ila aliyevaa jezi namba 11 (Miquissone), alikuwa hatari sana kwetu kwa sababu ametengeneza nafasi nyingi"
"Kwenye soka kuna matokeo matatu, tunakubali na sasa tunarejea nyumbani," alisema Nya
Miquissone alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo ambao uliwashuhudia Simba wakitinga raundi ya kwanza na sasa wakiwasubiri Platinum Fc tayari kwa mchezo wa kwanza ambao utapigwa nchini Zimbabwe Dusemba 23