Winga wa Simba Bernard Morrison amesema wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano ya Kimataifa msimu huu
Juzi Morrison alikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilicholazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Plateau United Simba ikifuzu raundi ya kwanza kwa faida ya ushindi wa bao 1-0 waliopata katika mchezo wa kwanza uliopigwa kule Nigeria
Baada ya kuvuka hatua hiyo ya awali, Simba itakumbana na Platinum Fc kutoka nchini Zimbabwe, mchezo wa kwanza ukipigwa Disemba 22-23 huko Zimbabwe
Morrison amesema wataendelea kuwapa furaha mashabiki wao ambao wameendelea kuwaunga mkono kila wanaposhuka dimbani
"Ninaona kwamba mashabiki wanafurahi kuona tunasonga mbele hata sisi pia tunafuraha, kikubwa ambacho tunakwenda kukifanya ni kuongeza juhudi kwa ajili ya mechi zetu zijazo
"Malengo yetu ni kuona tunafika mbali na hili linawezekana ikiwa kila mmoja anatimiza wajibu wake na ndicho tunachokwenda kukifanya," alisema Morrison
Β