Klabu ya Namungo Fc imefuzu raundi ya kwanza ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya CAF kufuta mchezo wao wa marudiano dhidi ya Al Rabita Fc kutoka Sudan Kusini baada ya Shirikisho la soka la nchi hiyo kushindwa kukamilisha taratibu kuhusu waamuzi
Namungo ilishinda mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Azam Complex, na mchezo wa marudiano ulikuwa upigwe hapo hapo Azam Complex baada ya Al Rabita kuomba kutokana na hali za kiusalama nchini Sudan
Baada ya uamuzi huo wa CAF, Namungo Fc itapewa ushindi na hivyo inatinga raundi ya kwanza na kufanya Wawakilishi wote wa Tanzania kuvuka raundi ya kwanza
Mabingwa wa Tanzania Simba wao walikuwa wa kwanza kutinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa ushindi wao wa bao 1-0 kule Nigeria ukiwavusha licha ya jana kulazimishwa suluhu ya bila kufungana