Kuwa shabiki wa Simba kwenye kizazi hiki ni raha sana, kwani unapoenda uwanjani au hata ukiwa nyumbani ukimshuhudia mnyama kupitia runinga, huwezi kujutia
Wachezaji wa Simba wa kizazi hiki wanaweza kuingia kwenye historia kuwa miongoni mwa kizazi bora kilichofanya mambo makubwa
Jana katika mchezo dhidi ya Plateau United, jina la winga Luis Miquissone ndilo lililozungumzwa zaidi
Mwamba huyu alifanya mambo ambayo ni nadra sana kuyaona katika soka la Afrika
Mwenyewe Wanamsimbazi wanasema mtu aliyemleta Miquissone Msimbazi moja kwa moja anaenda peponi (utani)

Kuna wakati safu ya ushambuliaji ya Simba ilipoa lakini sio kwa Miquissone
Aliwapa wakati mgumu Plateau muda wote wa mchezo, hakika walishukuru baada ya mchezo kumalizika kwani Miquissone aliwaweka kwenye presha kubwa
Ni bahati mbaya Simba haikupata ushindi lakini kwa hakika kiwango alichoonyesha Mmakonde huyu, kilistahili zawadi ya ushindi mnono
Huyu Miquissone ni silaha muhimu sana ya Simba katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu
Bosi Mo ajiandae kupokea ofa nono kutoka kwa vigogo wa soka barani Afrika na hata nje ya nchi kwani wachezaji aina yake ni wachache sana