Mabingwa nchi Simba wametinga raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa licha ya kulazimishwa suluhu ya bila ya kufungana dhidi ya Plateau United katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Simba imetinga raundi ya kwanza kwa ushindi wa jumla wa bao 1-0 matokeo waliyopata kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa kule Nigeria wiki iliyopita
Pamoja na kutengeneza nafasi nyingi, utulivu ulikosekana eneo la ushambuliaji huku walinzi wa Plateau United wakifanya kazi ya ziada kuepuka kipigo
Kwa mara nyingi winga Luis Miquissone amedhihirisha thamani yake akionyesha kiwango cha juu ambapo hakuna shaka anastahili kupewa tuzo ya nyota wa mchezo
Plateau waliunza mchezo huo taratibu, lakini wakabadilika katika kipindi cha pili wakijaribu kusaka bao la ugenini bila ya mafanikio
Simba sasa inakwenda raundi ya kwanza ambako inakwenda kuchuana na Platinum Fc ya nchini Zimbabwe
Platinum wao wameshinda mchezo wao kwa mabao 2-0
Baada ya kutinga raundi ya kwanza, Simba imebakiza kikwazo kimoja tuk kuelekea makundi




