Twendeni kwa wingi tukawaunge mkono wachezaji wetu - Barbara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Dec 2020
Twendeni kwa wingi tukawaunge mkono wachezaji wetu - Barbara

Mtendaji Mkuu wa Simba Barbara Gonzalez amewataka mashabiki wa Simba kuhakikisha leo wanajitokeza kwa wingi katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Plateau United

Mchezo huo wa marudiano utapigwa saa 11 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Barbara ambaye jana alifika uwanja wa Mo Simba Arena kushuhudia maandalizi ya mwisho, amesema Simba inajivunia kuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja hivyo ana imani leo hawatawaangusha mashabiki Wanamsimbazi watakaokwenda uwanjani kuwaunga mkono

"Faida yetu kwenye Ligi ya Mabingwa tuna wachezaji wenye uwezo mkubwa. Twendeni uwanjani kwa wingi tukawatie moyo timu yetu. Dhamana waliyonayo wachezaji wetu ni kubwa sana na hasa siku ya leo wanapokwenda kupambana na timu ya Plateau United," aliandika Barbara kwenye ukurasa wa mtandao wake wa kijamii

Jana Barbara alionekana kuwapa hamasa wachezaji waliokuwa wakikamilisha maandalizi uwanja wa Mo Simba Arena pale Bunju

Jioni ya leo wana kazi moja tu, kuipeleka Simba raundi ya kwanza ya michuano ya ligi ya mabingwa, wakiwa tayari wana faida ya ushindi wa bao 1-0 waliopata kule Nigeria

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’