Kila la kheri Mnyama, Kila la kheri Mwakilishi wa Nchi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Dec 2020
Kila la kheri Mnyama, Kila la kheri Mwakilishi wa Nchi

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo wana jukumu la Kitaifa pale uwanja wa Benjamin Mkapa watakapoikabili Plateau United kutoka nchini Nigeria katika mchezo wa ligi ya mabingwa

Mchezo huo ni wa marudiano Simba ikishinda bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita kule Nigeria

Kocha Mkuu wa Simba Sven Vandenbroeck amewataka mashabiki wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono timu yao

Amesema mchezo hautakuwa mwepesi kwa kuwa timu hizo zinatofautiana kwa bao moja tu, Simba ikiwa na faida ya kufunga bao hilo lililowapa ushindi ugenini

"Utakuwa mchezo mgumu, ni mchezo ambao tumepishana kwa goli moja hivyo lazima tuwe makini na natarajia mashabiki watajitokeza kwa wingi kutushangilia. Timu yao ni nzuri hivyo tunahitaji kila aina ya nguvu ambayo tunayo ili tupate matokeo mazuri," alisema Sven katika maandalizi ya mwisho jana

Kimahesabu, Simba inahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ili iweze kutinga raundi ya kwanza. Kucheza katika uwanja wa nyumbani mbele ya mashabiki wao 30,000 kutawaongezea wachezaji ari ya kupambana kuhakikisha wanapata matokeo

Ni utamaduni kwa Simba kuwa ni mwiko kufungwa wanapocheza uwanja wa Benjamin Mkapa, dua za kila Mwanasimba na Watanzania weledi wanaofahamu umuhimu wa Simba kufanya vizuri, wote wanaomba Simba ipate ushindi leo

Kikosi cha kocha Sven kiko kamili, hakuna wachezaji majeruhi hivyo matarajio ni makubwa kuwa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni, utawaacha Wanamsimbazi na furaha baada ya dakika 90

Nusu ya vita ilipiganwa kule Nigeria na Simba kushinda, leo Mnyama anakamilisha nusu nyingine iliyobaki, hakuna shaka hii pia atashinda

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’