Kaduguda afunguka mkakati wa usajili Ligi ya Mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Dec 2020
Kaduguda afunguka mkakati wa usajili Ligi ya Mabingwa

Wakati kesho Jumamosi Simba ikitarajiwa kushuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Plateau United katika mchezo wa marudiano michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Kaimu Mwenyekiti wa Simba Mwina Kaduguda, amefunguka mikakati ya usajili kwa ajili ya michuano hiyo

Kaduguda amesema lengo la Simba msimu huu ni kufika nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa zaidi barani Afrika katika ngazi ya vilabu

Amesema wanahitaji kuwa na kikosi kilichokamilika kila idara kuweza kutimiza malengo hayo

"Tumejipanga kuimarisha maeneo ambayo kocha amependekeza yaimarishwe. Umeona tumesajili kiungo mkabaji (Taddeo Lwanga) ambaye amechukua nafasi ya Fraga tuliyemsafirisha kwao Brazil ili akapate matibabu ya uhakika zaidi," alisema

"Lakini nafikiri yapo maeneo mengine ambayo tutaboresha hasa nafasi ya ulinzi na ushambuliaji. Unajua Mugalu (Chris) amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara, hivyo tunadhani huko mbeleni jambo hilo linaweza kutusumbua tukiwategemea washambuliaji hawa waliopo pekee"

"Kama malengo yetu yatafanikiwa, tutacheza zaidi ya mechi kumi mpaka kufikia hatua ya nusu fainali, ni lazima tuwe na kikosi imara ambacho kina wachezaji zaidi ya mmoja katika kila nafasi," aliongeza Kaduguda

Miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa huenda akarejea ni Mganda Emmanuel Okwi aliyeondoka msimu uliopita akijiunga na Al Ittihad ya nchini Misri

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) limeziruhusu timu zinazoshiriki michunao ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho kusajili wachezaji 40

Aidha TFF imeruhusu Simba kusajili wachezaji watano zaidi wa kigeni ambao hata hivyo hawatashiriki mechi za ligi kuu kama watakuwa nje ya idadi ya nyota 10 wanaoruhusiwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’