Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Plateau United ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Wakati akihojiwa katika kipindi cha Michezo cha EFM, Manara amesema Wanasimba wajitokeze kwa wingi kuiunga mkono timu yao katika mchezo huo muhimu lakini wahakikishe hawashiriki katika matukio yoyote ya uvunjifu wa Amani
"Wanasimba wenzangu nawaomba msiwapige wala kuwabugudhi mashabiki wengine wasio wa Simba kwenye mchezo wetu wa kesho, waacheni waje washuhudie soka safi na mpira ukiisha watafute pa kuziweka jezi zao. Kikubwa sisi tujitokeze kwa wingi kuishangilia timu yetu nina uhakika tutashinda," alisema Manara
Katika mchezo huo, Simba itaingia dimbani ikiwa na mtaji wa bao moja walilofunga kule Nigeria na kuondoka na ushindi wa bao 1-0
Wapinzani wao Plateau United wanatarajiwa kuwasili nchini leo tayari kwa mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa 11 jioni