Mpenja kunogesha tiki-taka kwa Mkapa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Dec 2020
Mpenja kunogesha tiki-taka kwa Mkapa

Mtangazaji mahiri wa kabumbu nchini Baraka Mpenja ndiye atakayesimamia 'shoo' ya keshokutwa Jumamosi pale uwanja wa Benjamin Mkapa wakati mabingwa wa nchi Simba wakipepetana na Plateau United katika mchezo wa marudiano hatua ya awali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Simba itaingia katika mchezo huo ikiwa tayari na mtaji wa bao moja, ushindi muhimu walioupata nchini Nigeria siku chache zilizopita

Mpenja ametangaza mechi nyingi kubwa za Simba na mara nyingi Mnyama ameunguruma katika mechi hizo

Mechi ambayo Wanamsimbazi wataendelea kuikumbuka kwa miaka mingi ni ile dhidi ya Nkana Fc ambayo Simba ilifunga bao lililowapeleka makundi dakika za usiiku kupitia kwa Clatous Chama 'Mwamba wa Lusaka', Mpenja akisherehesha ushindi huo wa kihistoria

Pengine Jumamosi ataongeza historia nyingine pale Simba watakapokuwa wakisaka ushindi utakaowapeleka raundi ya kwanza ya michuano hiyo msimu huu

Β 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’