Hatutawadharau Plateau United - Kaduguda

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
3 Dec 2020
Hatutawadharau Plateau United - Kaduguda

Huku ikimtambulisha kiungo mpya Taddeo Lwanga kutoka Klabu ya Tanta ya Ligi Kuu Misri na timu ya Taifa ya Uganda, uongozi wa Klabu ya Simba umesema kamwe hautawadharau wapinzani wao kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Plateau United kutoka Nigeria

Aidha, Simba ambayo itarudiana na Wanigeria hao Jumamosi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam, imesema lengo lao ni kuingia uwanjani kupambana mwanzo mwisho ikisaka ushindi wa kishindo sambamba na kuonyesha 'Tiki-taka' kwa mashabiki wao na wapenzi wa soka nchini kwa ujumla.

Tiki-Taka ni staili ya Kihispania ya uchezaji soka la pasi fupi na kupenyeza mpira katika nafasi mbalimbali likienda sambamba na kumiliki zaidi mpira.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini jana, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Mwina Kaduguda, alisema wanajipanga kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo huo wa maruadiano ili kuvuka hatua hiyo ya awali na endapo wataibuka na ushindi, Simba watacheza na mshindi wa jumla kati Costa do Sol ya Msumbiji ama FC Platinum ya Zimbabwe ambayo nayo ilipata ushindi wa mabao 2-1 katika mechi ya awali ugenini.

Alisema hii ni mara ya kwanza kwa timu kutoka Tanzania kushinda ugenini katika ardhi ya Nigeria, hivyo wanahitaji kupambana dakika 90 zingine kutafuta ushindi, ili kufikia malengo yao ya kusonga mbele ya michuano hiyo na kufika nusu fainali.

"Hatutabweteka, mimi najua mpira wale jamaa ni wazuri, tunatakiwa kupambana dakika 90, tunafanya jitihada za kuhakikisha hawatoki katika uwanjani wetu wa nyumbani.

"Hatusikilizi propaganda kwamba wapinzani wetu ni wa kawaida maana ni mabingwa wa Nigeria tukumbuke amemfunga Enyimba ambaye ni mabingwa mara tatu, kila mmoja anajua ubora wa Enyimba," alisema Kaduguda.

Kaduguda pia hakusita kuipongeza Bodi ya Wakurugenzi wa Simba chini ya Mwenyekiti wao, Mohamed 'Mo' Dewji, kwa kujitolea kusaidia klabu hiyo hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa mabadiliko.

Alisema Mo Dewji amefanikiwa kutoa Sh. milioni 700 kuhakikisha anamwongeza mkataba Clatous Chama kuendelea ili kubaki ndani ya klabu hiyo.

"Ukimtoa Chama, hivi leo (jana) tumetambulisha nyota mpya Mganda Taddeo Lwanga ambaye anakuja kuchukuwa nafasi ya Gerson Fraga," alisema Kaduguda.

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
29m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
22h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’