Uongozi wa klabu ya Simba umetaja viingilio vya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Plateau United ambao utapigwa Jumamosi uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza na Wanahabari Serena Hoteli mapema leo, Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara ameweka hadharani viingilio vya mchezo huo
Platinum ni Tsh 150,000/-, VIP A Tsh 40,000/-, VIP B na C Tsh 20,000/- na Mzunguko Tsh 7000/-. Manara amesema tiketi zimeanzwa kuuzwa leo na mashabiki wanaotakiwa kuhudhuria ni 30,000
Manara amebainisha kuwa Jumamosi utapigwa mpira mkubwa, kauli mbinu yake ikiwa ni soka tiki-taka
"Tunakwenda na kauli mbiu ya tiki-taka kwa Mkapa, kila mmoja wetu, mwanasimba ajue kauli mbiu ni tiki-taka kwa Mkapa"
Manara amesema anatarajia kuona mashabiki wa Simba wakijitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao lakini ikitokea kuna mashabiki wa Yanga wamepenya, wasipigwe kwani kwa soka litakalotandazwa, wataondoka wenyewe!
"Ikitokea bahati mbaya mmoja wao amepenya kwenye uwanja kuja kutuzomea asipigwe, pira biriani litakalopigwa linaweza kumtia wazimu mwenyewe akaondoka"