Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amesema wanaandaa utaratibu wa kuhakikisha mashabiki wa Simba hawabugudhiwi kwenye mchezo wa marudiano ligi ya mabingwa dhidi ya Plateau United
Mchezo huo utapigwa mwishoni mwa wiki uwanja wa Benjamin Mkapa
Mashabiki takribani 30,000 wataruhusiwa kuushuhudia mchezo huo, Manara akibainisha kuwa watahakikisha ni Wanasimba watakaopata nafasi ya kuingia uwanja wa Mkapa
"Hizi Shumizi zenu bado mnazo Utopolo? Okey, Mtazivalia makwenu.Tutaandaa utaratibu maalum utakaohakikisha Washabiki wote 30,000 watakaoingia uwanjani katika mechi ya marudiano ni Washabiki wa Simba," Manara aliwapiga kijembe mashabiki wa Yanga ambao walivalia jezi za Plateau United
Baada ya ushindi ugenini, huu ni mchezo ambao Simba itahitaji kumaliza kazi kabisa nyumbani kuhakikisha wanatinga raundi ya kwanza ambao itakuwa hatua moja kuelekea makundi au kucheza raundi inayofuata ya michuano ya kombe la Shirikisho